23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Lambart ahoji MSD kuzalisha dawa kabla ya sheria kupitishwa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mbunge wa Viti maalumu, Agnesta Lambart amehoji juu ya Bohari ya Dawa nchini (MSD) kuanza uzalishaji wa dawa kabla ya sheria pitishwa na bunge.

Aidha, Lambart alihoji sababu za kiwanda hicho kutengeneza dawa ilihali kwamba ufanisis wake uko chini.

Hatua hiyo imezua ilizua mvutano baina ya mbunge huyo na Spika wa bunge, Job Ndugai, kwenye kikao hicho cha bunge la 12 linaloendelea jijini Dodoma.

“Mheshimiwa Spika naomba niende moja kwa moja katika sehemu ya nne katika sheria ya Bohari ya Madawa kuuliza ni kwa tetesi zilizopo MSD imeanza kufanya uzalishaji wa dawa wakati sheria bado haijapitishwa,”alihoji mbunge huyo.

Aidha, aliongeza kuwa MSD ilionesha udhaifu katika usambazaji wa dawa na kwamba ilishindwa kufanya kazi kwa weredi iweje leo waongezewe kazi nyingine ya kuzalisha dawa.

Wakati Mbunge huyo akiendelea kuchangia mswada huo Namba Nne wa Sheria ya MSD, Spika Ndugai aliingilia kati mchango huo na kutaka kujua anasoma katika eneo gani, lakini licha ya mbunge huyo kumtajia, alimwambia wako bungeni kutunga sheria siyo kuzungumzia tetesi.

“Kwanza unasoma wapi? mbona sielewi? Sisi hapa tuko kwa ajili ya kutunga sheria siyo kuzungumzia tetesi, alafu uhwezi kuendelea mpaka uniambie hicho unachokisoma kiko ukurasa gani,” alihoji Ndugai huku akionekana kukerwa na taarifa hiyo.

Lambart alisema kuwa katika mswada huo MSD inahitaji kufanya uzalishaji wa dawa na vifaa tiba.

Amesema MSD ilishindwa kusambaza dawa nchi nzima lakini kwa mawazo yake haoni kama ina uwezo wa kufanya mambo yote kwa wakati mmoja.

“Najua licha ya kupinga sheria hiyo, lakini najua sheria hiyo itaenda kupita, lazima nisema ukweli,” amesema Lambart.

Aidha, wakati Lambart akiongea hayo Spika Ndugai alisema kwa sababau hajaelewa lakini akieleweshwa ataelewa MSD kama ikizalisha baadhi ya dawa hapa nchini itaokoa mabilioni ya pesa zilizokuwa zikipotea kwa kuagiza dawa nje ya nchi.

Hata hivyo, mbunge huyo alisimamia katika kauli yake hiyoh kuwa MSD walishindwa kusambaza dawa hayo na hata yeye anajua hivyo hawezi kuzalisha dawa hizo kwa weredi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles