25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Kuziba pengo la kidijitali kulivyobadili maisha ya wanawake

Kina mama wa wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wakipatiwa simu za mkononi na kampuni ya Tigo.
Kina mama wa wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wakipatiwa simu za mkononi na kampuni ya Tigo.

Na Mwandishi Wetu,

KATIKA mkutano wa Umoja wa Kampuni za Simu uliomalizika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ilibainishwa kwamba maisha ya wanawake wengi nchini hususani wale wanaoishi maeneo ya vijijini  yanaweza kubadilishwa kwa kiwango kikubwa na kuwa mazuri  kama watakuwa wameunganishwa vizuri kidijitali.

Mtazamo huo uliungwa mkono na utafiti uliofanywa na Kampuni ya Simu ya Tigo na Kampuni ya Kidogo Kidogo  inayojishughulisha na ujasiriamali jamii  yenye makao yake nchini Marekani. Kampuni hii ilianzishwa kwa lengo la kusaidia kupunguza tatizo la pengo la kidijitali  katika simu kwa hatua za taratibu  kwa kusaidia  kutoa simu za bure  kwa wanawake walio na kipato cha chini.

Katika jaribio lililofanywa  simu za mkononi ziligawiwa kwa washiriki kupitia  warsha iliyotoa mafunzo ya teknolojia ya simu. Washiriki walipokea maelezo  kuhusu namna ya kutumia simu mpya aina ya Nokia 105 kupitia huduma zilizotolewa na Tigo.

Utafiti huo uliofanywa kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la CARE International, Shirika la Utafiti wa Kupunguza Umaskini (Repoa) ambalo linaongoza kwa utafitri katika Nyanja hiyo Tanzania na watafiti kutoka Chuo cha William and Mary na Chuo Kikuu cha Brigham Young nchini Marekani  ambao ulijumuisha  zaidi ya wanawake 400 kutoka wilaya za Rufiji, na Kilwa  katika ukanda wa pwani ya Tanzania.

Aidha, utafiti huo  ulikuwa na kipindi cha miezi sita ya  kufanya tathmini  ukiwa na mtazamo katika kumiliki na kutumia simu ya mkononi na kuangalia matokeo yake katika ustawi na uwezeshwaji kwa mtu binafsi.

Makundi hayo matatu ya utafiti yalijipanga na jumla ya washiriki 150 walipokea simu pamoja na kadi za simu za Tigo zikiwa na salio la kutosha  wakati wa kuanza kwa utafiti Desemba 2015 wakati washiriki 100 walipewa fedha taslimu kwa uwiano sawa na hawakupewa simu.

Kundi jingine la washiriki 150  wakiwa ni kundi lililokuwa chini ya udhibiti walipokea simu baada ya  kumalizika kwa utaifi Julai 2016.

Warsha za ufuatiliaji wa utafiti  ziliendeshwa na mdau wa ndani ambao ni  Chama cha waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET).

Hakuna aliyekuwa anamiliki simu  wakati utafiti huo ulipokuwa unaanza na wengi wao walikuwa ni wakulima wadogo, wakiwa na umri  kati ya miaka 18 hadi 79. Miongoni mwao  asilimia 35 ya washiriki  walikuwa hawana weledi wa aina yoyote kwa kuwa walikuwa hawajui kusoma wala kuandika, asilimia 24  angalau walikuwa na weledi kidogo  na asilimia 38 walikuwa ni weledi.

Asilimia 91 ya washiriki  awali walisema kuwa  gharama za kifedha kwa ajili ya kununua simu  zilikuwa  kubwa na hivyo kuwa kikwazo kwao kumudu kununua simu. Hivyo, kwa kupata simu za bure  mabadiliko chanya yameonekana.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali ya utafiti, wamiliki wa simu za mkononi  walipata matokeo kadhaa chanya  miongoni mwa wanawake ambayo yalijumuisha  kuweza kuifikia mitandao ya kijamii, taarifa za kifedha na kuongeza kipato  cha wiki na mwezi katika biashara zao ndogondogo.

Hali halisi

Hali inayofahamika baya na ni kwamba mwanamke wa kawaida barani Afrika  yupo nyuma kidijitali katika enzi hizi ambapo wanawake katika mabara mengine  wapo katika mkondo sahihi wa sekta hiyo na wanakimbia, hata hivyo  ubunifu wa kubadilisha maisha  ulioletwa na simu  za mkononi kama vile zana za  huduma ya afya, kuhamisha fedha.

Kutokana na hali hiyo  ni muhimu kufikiria jinsi  kujumuishwa kidijitali, huduma za fedha kwa simu za mkononi  kama vile huduma ya Tigopesa  itakavyoibadili Afrika  kwa ujumla, hususani kwa Tanzania. Inatakiwa kukumbuka kwamba kupata taarifa  imetajwa katika mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez alipongeza matokeo chanya ya teknolojia ya simu  ambao umeletwa Afrika  na kubainisha maeneo manne ambayo  yanatakiwa kushughulikiwa  ili kuongeza  ujumuishwaji kidijitali.

“Kuna vikwazo vikubwa katika kuridhia, hususani kwa makundi ya jamii ambayo ni maskini  kama vile maeneo  ya vijijini, wanawake walio na kipato cha chini na vijana,” alisema.

Kama mdau katika sekta hiyo kwa haraka alidokeza  simulizi kadhaa za mafanikio  ikiwa ni pamoja na kukua kwa  huduma za simu, ikiwmao fedha, afya (mHealth) nakilimo (mAgri).

Maeneo ya mtandao yanaweza kuboreshwa kwa  kupanua mitandao ya simu  yenye uwanda mpana kuyafikia makundi ya jamii ambayo ni maskini. Hadi hapo ndipo kampuni imeweza kuondokana na adha hiyo kupitia uendeshaji wa pamoja  na mitandao mingine  na moja kwa moja  kuinunua Zantel  ili kuwafikia watu wa Zanzibar  na Mkoa wa Pwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,763FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles