32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

KUSHIKILIWA NDEGE YA ATCL: Waziri afanya vikao hadi usiku wa manane

  • AG aongoza jopo la mawakili wa Serikali Afrika Kusini

ASHA BANI -DAR ES SALAAM

JOPO la mawakili wa Serikali likiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) limewasili Afrika Kusini tayari kwa kuanza mazungumzo ya kisheria ili ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) iachiwa mara moja.

Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Mafia na Nyamisati,

Alisema tukio hilo limemsikitisha yeye na Watanzania wote.

Alisema tangu alipopata taarifa za kushikiliwa  kwa ndege hiyo hakulala mpaka saa nane usiku akiwasikiliza wanasheria waliokuwa wakitoa ushauri jinsi ya kupata  suluhi ya kisheria.

“Nilipata taarifa hii, nilikaa na wanasheria wetu hadi saa nane usiku tukijadiliana namna ya kupata ufumbuzi wa kisheria.

“Mpaka leo (jana), tayari  AG na jopo la mawakili ameanza  safari ya kwenda Afrika Kusini ili kuzungumza na wenzetu.

“Ndege  imeshikiliwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya Afrika Kusini, hata sisi kabla ya kushikiliwa kwake hatukua na taarifa, wala hawakutupa taarifa mapema, ni tukio la ghafla ilikuwa siku ya mapumziko imeanza, hatukuweza  kufanya mawasiliano kiofisi kwa kuwa zilikuwa ni siku za mapumziko kiserikali kama ilivyo kwa nchi zingine duniani.

“Lengo letu ndege iachiwe haraka iiendelee na safari zake,tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali nimezungumza naye na jopo limekwenda kuzungumza kisheria kuona jinsi ndege hiyo itakavyoachiwa,”alisema.

Alisema hata wakati wanafanya mazungumzo hayo jana, walikuwa ana wanasheria pamoja na balozi mdogo wa Afrika Kusini  wakifanya mazungumzo na mambo yalikwenda sawa.

Alisema ameshangaa na dunia imeshangaa kwa kuwa Tanzania haina ugomvi wowote wa kibiashara na Afrika Kusini na kwamba nchi iliwahi kuipigania kutafuta uhuru wake hakuna asiyejua hilo.

Alisema mpaka sasa hafahamu chanzo cha kuzuia kwake kwa kuwa hakuna ugomvi uliopo baina ya nchi hizo.

Alisema kama kungekuwa na ugomvi hata Tanzania ingeweza kuzuia ndege zake ambazo kwa siku zinatua mara mbili hapa nchini.

“Kwa siku ndege za Afrika Kusini zinatua mara mbili, hata leo (jana), asubuhi imetua, saa tisa inatua tena, tungekuwa na ugomvi wowote basi wangeweza kuzikamata ambazo zipo muda wote,”

Alisema safari ya wasafiri waliokwama imeanza jana na leo kwa kutumia ndege ya Afrika Kusini.

“Baada ya hapo ikabidi kuànza mazungumzo na makampuni mengine ya ndege ili  ambapo tulizungumza na kampuni ya Rwanda Air Aways na Ethiopia air ways walikataa ikabidi kuanza mazungumzo na kampuni ya Afrika Kusini iliyotukubaliana na kuanza kusafirisha abiria na mizigo yao jana na leo,” alisema Kamwelwe.

Mhandisi  Kamwele aliwataka Watanzania kuwa na subira na kuahidi kupitia wanasheria waliokwenda huko watakuwa wanatoa taarifa kila baada ya muda.

Alisema Serikali iko imara na makini na kwamba sekta ya anga imefanikiwa kwa asilimia 75 kupata abiria inapokuwa katika safari zake.

Alisema kuna ndege kubwa mbili zinatarajia kuwasili nchini mapema mwakani.

KIVUKO

Wakati huo huo,Waziri Kamwelwe alizindua kivuko cha Nyamisati na Mafia na kusema kitaanza safari zake  Machi, mwakani.

Kivuko hiko kitagharimu Sh bilioni 5.3 bila VAT na ni fedha za serikali zilizotokana na kodi ya Watanzania.

Alisema Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), ndiyo waliofanikisha hilo ambapo kikikamilika kinafanya jumla ya viviko 30 katika vituo (ferry stations 20 )Tanzania Bara.

Mbunge wa Mafia, Mbaraka  Dau alisema ilikuwa changamoto kubwa kwa wananchi kutokana na kukosa kivuko cha uhakika.

Aliishukuru Serikali kutoa fedha kwa muda muafaka kwa mkandarasi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport ili akamilishe kazi kwa muda muafaka walioupanga wao ambao ni Februari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles