29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kunenge awahimiza Ma-DC wapya kuheshimu wa watakaowakuta

Na Brighiter Masaki, Pwani Kibaha

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakari Kunenge, amewaapisha wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Pwani, baada ya kuteuliwa Juni 19, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Wakuu wa Wilaya wapya walioapishwa na Kunenge leo Jumatatu Juni 21, 2021 ni Nickson Simon, (Kisarawe) na Sara Msafiri, (Kibaha) Zainabu Issa, (Bagamoyo), Khadija Ali (Mkulanga) na Stephens Gowelle, (Mafia) ambaye hakuweza kuapishwa kutokana na matatizo ya kiafya wakiendelea na majukumu yao ya awali.

Baada ya uapisho huo, Kunenge, amewataka Wakuu hao kufanya kazi kwa bidii katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa na Rais Samia, amesema rais anafahamu eneo kubwa la nchi ya Tanzania hivyo kuwa na imani nao katika nafasi hiyo ya uwakilishi wa ukuu wa wilaya.

“Nimefurahi kupata wakuu wa wilaya wapya, niwakaribishe kufanya kazi kwa ushirikiano bila kuangalia tofauti za umri, naamini hawa wengine ni wazoefu katika majukumu yao hivyo natarajia mtafundishana kazi ili twende sawa”, amesema Kunenge

Amewataka wakuu hao wa wilaya kufika kwenye vituo vyao vya kazi na kutoa ushirikiano kwa watendaji waliowatangulia katika vituo hivyo.

“Mkifika kwenye maeneo yenu ya kazi hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii na ushirikiano, rais amewaleta katika mkoa huu naamini ana matarajio na wote,” Kunenge.

Kwa upande wake, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson Simon akizungumza kwa niaba ya wenzake, amemshukuru rais kwa nafasi aliyompatia na ameomba ushirikiano kwa sehemu walizopangiwa na rais ili kufanikisha azma na matakwa ya serikali ya Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles