23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Kuna upungufi sekta binafsi-Manyanya

 FARAJA MASINDE– DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema sekta binafsi nchini bado ni ‘dhaifu’ hatua ambayo inafanya uwekezaji ushindwe kufanyika kikamilifu kama lilivyo lengo la Serikali la kufikia uchumi wa kati unaochangizwa na viwanda.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, wakati akifanya mahojiano wakati wa kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na kituo cha luninga cha Star Tv.

Alisema bado kuna changamoto kubwa katika kuhakikisha kuwa sekta hiyo inanyanyuka na kuwa kiungo muhimu kwa maendeleo ya serikali, huku akisisitiza kuwa pamoja na serikali kujaribu kuisaidia kwa kutoa mitaji kwa baadhi ya wawekezaji lakini bado tija yake imekuwa kinyume na matarajio.

“Mkakati wa Serikali ni kuona viwanda vinaimarika na kufanya kazi kwa ufanisi,nikiri changamoto bado ni kubwa, ndiyo maana tunandelea kuimarisha sekta binafsi yetu iliyopo ambayo inahusisha wananchi wenyewe, changamoto sekta binafsi yetu iliyopo bado ni dhaifu haijaweza kuwa na nguvu kubwa ya kuwekeza.

“Serikali tunaendelea kuona namna nzuri ya kushirikiana na sekta binafsi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa, ni wazi ni injini ya uchumi, unapokuwa na sekta binafsi ambayo ni legelege hutaweza kufika unakotaka kwenda na utabaini kuwa inakwamba kwenye mitaji japo kuna wakati serikali ilijaribu kuwakopesha mitaji baadhi, matokeo yake hayakuwa kama Serikali iliyotarajia,” alisema.

Alisema katika ‘udhaifu’ huo, hakupaswi kulaumiana badala yake kunatakiwa kujifunza na kuangalia mbinu mbadala za kuikwamua.

“Tumewahi kuwaita watu wa sekta binafsi mara kwamba mara ukiacha ile waliyokaa na Rais Dk. John Magufulu, tuliongea na kuchambua matatizo yaliyopo na tukasema kuwa ni lazima tushirikiane pale penye changamoto tuzindoe, pale penye usaidizi ufanyike.

“Pengine itafikia mahali hata Serikali itachangia wataalamu mfano wawili na kiwanda kikishasimama basi wanaondoka, tayari Serikali inaendelea kusomesha wataalamu, tumeona kuna mbinu mbalimbali ambazo tunadhani kuwa ni lazima kuzitumia ili kunyanyua sekta binafsi nchini, kwani mtu anaweza kuwa na fedha ya kuanzisha kiwanda lakini wataalamu hana,” alisema Mhandisi Manyanya.

Kuhusu kuongezeka kwa raia wengi wa kigeni kwenye viwanda mbalimbali hususan vile vinagvyomilikiwa na raia wa bara la Asia, ambao wanafanyakazi zinazowezwa kufanywa na wazawa, Manyanya alisema suala hilo lina mambo mengi.

“Jambo hili lina mitizano ya aina mbili, kwa maana ya kitaalamu na kwa mapana ya nchi, unajua kuna mambo ambayo ni kama yanakinzana, unajua kwenye viwanda au biahsara nikwamba mwenye biashara anakuwa karibu sana na biashara yake.

“Unakutana mwenyebiashara kutokuwa na imani na mtu anayemweka pale, basi hata nguvu ya kuwekeza inakuwa ndogo kwa kuhofia kuwa anayemweka hapo anaweza akawa mwizi, eneo jingine ni utaalamu unakuta mtu anayeletwa ni mtaalamu anayeaminiwa na mwenye mali yake, kwa mazingira kama hayo tunasema wenzetu wanaohusika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles