25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Makazi ya sokwe mtu yageuzwa mashamba

 WALTER MGULUCHUMA– KATAVI

ATHARI za tabia ya mabadiliko ya tabia za nchi na watu kuvamia maeneo mengi yaliyokuwa makazi ya wanyama aina ya sokwe mtu wilaya za Tanganyika (Rukwa) ,Uvinza (Kigoma) na mkoani Rukwa miaka 20 hadi 50 iliyopita, sasa hivi makazi yamekuwa mashamba na makazi ya watu,zimesababisha wanyama hao kutoweka maeneo hayo .

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Sayansi na Utafiti wa Taasisi ya Jane Goodall, Dk. Shadirack Kamenya wakati wa maadhimisho ya miaka 29 tangu kuanzishwa kwa ROOTS &SHOOTS( mizizi na Chipukizi( yaliofanyika makazi ya wakimbizi ya Mishamo .

Alibainisha athari za mabadiliko ya tabia nchi, zimeathiri hata viumbe wengine kama sokwe mtu na wanyama wengine wengi chakula chao kikuu ni matunda mabadiliko ya tabia ya nchi yanaweza kuathiri upatikanaji wa maua.

Pamoja na athari hiyo, maeneo mengi ambayo yalikuwa makazi ya sokwemtu wilaya za Mkoa wa Kigoma, Tanganyika mkoani Katavi na Rukwa mika 20 hadi 50 iliyopita sasa hizi maeneo hayo yamekuwa ni mashamba na makazi ya watu .

Hali hiyo imefanya sokwe waliokuwapo kutoweka maeneo hayo, Tanaznia kuna wastani wa sokwe 2,500 wanaopatikana maeneo ya mikoa hiyo kama mpango mkakati wa uhifadhi wa sokwemtu usemavyo na watafiti wengine wanasema ni kati ya 2,200 hadi 2,600.

 Duniani sokwe mtu wanapatikana bara la Afrika peke yake, Afrika Mashariki kati na magharibi, yasemekana wamepungua kutoka milioni 2 mwaka 1990 ahdi 300,000 waliosalia

Alisema sokwemtu, ni rasilimali tunu za urithi wa taifa ,tabia zao zinafanya wawe kivutio kikubwa cha watalii ni mnyama wa pekee walio na tabia nyingi zinazofanana na binadamu. Alisema wana vinasaba kwa asilimia 90.8 kutokana na taarifa ya wanasayansi .

Alisema wakati wa wiki ya maadhimisho hayo,wanafunzi na walimu wa shule za msingi na sekondari 4,036 wamejiunga kuwa Roots and Shoots .

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Salehe Mhando alisema idadi kubwa ya Sokwe walipo nchini wanapatikana katika Mkoa wa Katavi. 

Alisema walipo nchini ni 2, 600, wanaopatikana Mkoa wa Kigoma ni 600, Rukwa 100 na wanaobaki wanapatikana kwenye mapori ya mistu ya Tongwe mashariki na magharibi katika wilaya hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika, Rojas Rumuli aliwataka wakazi wa wilaya kuiunga mkono taasisi ya Jane Goodoll katika jitihada wanazozifanya za kutunza mazingira.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles