23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

KOREA KASKAZINI: TUKO TAYARI KUACHANA NA NYUKLIA

BEIJING, CHINA


KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amemwambia Rais wa China, Xi Jinping, kwamba utawala wake uko tayari kuachana na matumizi ya silaha za nyuklia.

Shirika la Habari la China, Xinhua limeripoti hayo jana wakati ambao Kim ambaye ni mshirika wa China amefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi, kabla mikutano ya kilele na Korea Kusini na Marekani.

Hata hivyo, Kim amesema kuachana na silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea kunawezekana iwapo tu Korea Kusini na Marekani zitaitikia juhudi zao kwa nia njema, kuweka mazingira ya amani na utulivu.

Baada ya uvumi wa siku nyingi, hatimaye China na Korea Kaskazini zilithibitisha kufanyika kwa ziara hiyo, ambayo ni ya kwanza kwa Kim nje ya taifa lake tangu alipoingia madarakani mwaka 2011.

Kim alifanya ‘mazungumzo ya kufana’ na kiongozi wa China Xi Jinping mjini Beijing, Shirika la Habari la China, Xinhua liliripoti jana.

China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kiuchumi na baadhi ya wachambuzi walitabiri kukutana kwa wawili hao kabla ya Kim kukutana na marais wa Korea Kusini na Marekani.

Kim amepangiwa kukutana na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in Aprili na Rais wa Marekani Donald Trump Mei.

Ziara hiyo ya Beijing inatazamwa na wengi kama hatua muhimu katika maandalizi ya Korea Kaskazini kukutana na viongozi hao.

Kim alimhakikishia Rais mwenzake wa China kuwa amejitolea kuacha kustawisha silaha za nyuklia, kwa mujibu wa Xinhua.

Kim aliwasili akiandamana na mkewe, Ri Sol Ju, Jumapili na wawili hao waliondoka Beijing Jumanne alasiri, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles