23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kolabo ya Scorpion Kings, Tresor ni noma!

Na Mwandishi Wetu

Kundi la muziki kutoka Afrika Kusini, Scorpion Kings linaloundwa na wasanii, DJ Maphorisa na Kabza De Small, wametoa albamu ya nguvu iitwayo, ‘Rumble In The Jungle’ ambayo wamepiga kolabo na msanii mkali, Tresor.

Ni albamu yenye nyimbo 14 za ukweli ambazo zina mahadhi ya Amapiano, ambayo tayari inapatikana kupitia platforms mbalimbali mitandaoni.

Wakiwa kama wabunifu wakubwa wa midundo motomoto nchini Afrika Kusini kwa karibu miaka 10 iliyopita wakifanya kolabo na mastaa mbalimbali, kama DJ Maphorisa (Uhuru’s “Y-Tjukutja”, Mafikizolo’s “Khona” na “Midnight Starring”.

Kwa upande wa Kabza De Small amefanya “Sponono” na “iLog Drum”, wote wameendelea kusukuma muziki wa Afrika ulimwenguni kama mabalozi wakubwa wa ladha za Kiafrika.

Ukiachana na albamu hii, nyingine maarufu ni pamoja na Scorpion Kings (2019), Return of the Scorpion Kings (2019) na Scorpion Kings Live waliyoachia mwaka jana, 2020.

DJ Maphorisa anasema: “Albamu hii ni zawadi kwa Waafrika na dunia nzima. Tumeachia ladha ya Amapiano barani kwetu. Tunapenda kufanya kazi zinazogusa watu wetu, lakini wakati huohuo dunia nzima inapata ladha ya muziki mzuri.”

Tresor, yeye amekuwa akifanya mauzo makubwa ya muziki wake huku akishinda tuzo ya Albamu Bora ya Pop katika Tuzo za Muziki za Afrika Kusini (SAMAs – South Africa Music Award), mara tatu mfululizo.

Ndani ya albamu “Rumble In The Jungle” zinapatikana nyimbo zake mbili maarufu zaidi kwa sasa, “Funu” na “Fola Sade”.

Akizungumzia albamu hiyo, Tresor anasema: “Hii ni albamu nzuri, maalum na ya kipekee kwangu kwa sababu inadhihirisha utajiri wetu wa sauti na midundo mizuri ya Kiafrika. Tumerudi kwenye asili yetu na kuudhihirishia ulimwengu kuwa ipo albamu bora ya muziki wa Kiafrika kutoka nyumbani.”

Aliongeza: “Rumble In The Jungle ni albamu yenye kishindo cha sauti, daraja la kitamaduni linalovunja vizuizi vyote na kuwaleta watu wetu pamoja kupitia muziki. Tunachanganya mdundo wa Afrika Kusini wa Amapiano na sauti za Kiswahili, Kifaransa na Kikongo.

“Zaidi kuna vionjo vya mapigo ya Afrika Magharibi na vitu vya Afrobeats. Ni ya ujasiri juu ya ujasiri. Ni albamu isiyochosha hata kidogo. Ina ladha bomba.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles