23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

TAWA,WCS wakubaliana usimamizi wa pamoja miradi ya mfumo wa ikolojia

Na Victor Makinda, Morogoro

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Shirika lisilo la kiserikali la Uhifadhi wa Wanyamapori  “Wildlife Conservation Society” (WCS)  wamesaini hati ya makubaliano yenye lengo la kuhakikisha kunakuwa na usimamizi wa pamoja wa miradi mbalimbali katika mfumo wa ikolojia Ruaha, Katavi ambao unajumuisha mapori ya ya akiba ya Rungwa, Muhesi,Kizigo, Lukwati/Piti na Rukwa Lwafi.

Akizungumza katika hafla  ya makabidhiano iliyofanyika jana, ofisi za Makao Makuu ya TAWA Mkoani wa Morogoro, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi, Mabula Misungwi, aliwashukuru WCS kwa juhudi za dhati wanazofanya katika uhifadhi na mashirikiano yao na TAWA katika kuhifadhi rasilimali zilizopo katika maeneo wanayo yasimamia.

“Ujangili ni swala mtambuka ambalo linahitaji kuunganisha nguvu za pamoja, rasilimali na uzoefu katika kupambana nao na hivyo tunawaomba WCS msichoke katika juhudi kupambana nao na isiwe mwisho bali mwanzo wa ushirikiano wenu,” alisema Mabula.

Naye Mkurugenzi wa WCS Taifa, Noah Mpunga, aliwashukuru TAWA kwa ushirikiano wao wanaouonesha katika mapambano dhidi ya ujangili na kusisitiza kuwa ni muhimu kushirikiana na kwamba ili TAWA waweze kufikia malengo yao michango ya wadau wa Uhifadhi ni ya muhimu kwa uhifadhi endelevu.

“Ninawashukuru sana TAWA kwa ushirikiano wenu, pia ninawapongeza kwa kazi kubwa yenye tija kwa Taifa hili katika nyanja ya uhifadhi, Sisi WSC tunaahidi ushirikiano endelevu  kwani tunaamini kuwa bila ushirikiano madhubuti ni vigumu kufikia malengo,” alisema Mpunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles