29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Kocha Morocco aukubali mziki wa Cameroon.

NA MOHAMED MHARIZO

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya vijana ya Morocco Jamal Sellami, amesema Cameroon wana ligi nzuri za vijana na ndio sababu ya kuwa na timu bora. 

Sellami alisema hayo jana baada ya timu yake ya Morocco kufungwa mabao 2-1 na Cameroon, katika mchezo wa pili wa kundi B wa michuano ya Afrika kwa vijana walio na umri chini ya miaka 17, uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

 Alisema kuwa wachezaji wake walipamba na kutangulia kufunga, lakini makosa yakujirudiarudia kama ilivyokuwa katika mchezo wao na Senegal yaliwagharimu. 

 “Wachezaji wangu wameonyesha uwezo mzuri, hata mchezo uliopita na Senegal tulitangulia kufunga lakini walisawazisha.

 “Kwa hiyo ni makosa yaleyale yametugharimu, tulitangulia kufunga lakini tumefungwa,”alisema na kuongeza.

Naweza kusema wenzetu Cameroon wako vizuri tofauti na sisi kwani wao wana ligi nzuri za vijana.”

 Alisema kuwa, wamejifunza vitu vingi kwenye michuano hiyo na watakwenda kujipanga upya ili kuhakikisha wanafanya viuzri katika michuano ijayo. 

Cameroon kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Morocco, imetinga nusu fainali ya michuano hiyo ya vijana Afrika na kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil baadae mwaka huu.

 Cameroon imeungana na Nigeria kufuzu Kombe la Dunia, ambapo timu nne zitafuzu kwa fainali hizo kutoka Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles