21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Klopp: Liverpool wajilaumu wenyewe kutoa sare

jurgen-kloppLIVERPOOL, ENGLAND

BAADA ya klabu ya Liverpool kushindwa kutumia vizuri Uwanja wa nyumbani wa Anfield kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester United juzi, kocha wa klabu hiyo, Jurgen Klopp, amesema wachezaji wa Liverpool wanatakiwa kujilaumu wenyewe.

Kocha huyo ameyasema hayo baada ya klabu yake kushindwa kutumia nafasi walizozipata katika mchezo huo na kujikuta wakitoa sare ya bila kufungana.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo, Manchester United walionekana kuutawala mchezo lakini walikosa nafasi ya kupata bao au kufanya shambulizi la kutisha, lakini baada ya kipindi cha pili kuanza, Liverpool walionekana kuutawala mchezo huku wakitafuta bao la kuongoza.

Liverpool walipata nafasi nyingi za kutafuta bao, lakini walishindwa kuzitumia, hivyo kocha wa klabu hiyo amedai kuwa wachezaji wanatakiwa kujilaumu wenyewe kwa kushindwa kuzitumia nafasi hizo.

“Nimekuwa na hisia tofauti kutokana na mchezo huo na sina furaha kabisa, tumeshindwa kufanya vizuri nyumbani wakati nafasi tulikuwa nazo nyingi, hakuna wa kumlaumu zaidi ya sisi wenyewe.

“Naweza kusema tumecheza vizuri, lakini hatukukusudia kucheza kama vile, tulipata nafasi za wazi kama mbili au tatu, lakini mlinda mlango wao, David de Gea, alionesha kiwango cha hali ya juu na kuokoa mipira hiyo ya hatari.

“Sikuwa na wasiwasi na safu ya ulinzi kwa kuwa ilianza vema tangu dakika ya kwanza, lakini katika umaliziaji kulikuwa na tatitzo,” alisema Klopp.

Kwa upande wake kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, amedai kuwa Liverpool walikuwa na uwezo wa kawaida na ndio maana walishindwa kuutumia uwanja wao vizuri.

“Msimu iliopita, Manchester United ilishinda katika uwanja huu, wakati huo Liverpool wakiwa wamepiga mashuti 14 ambayo yalilenga langoni, lakini United ilipiga shuti moja ila iliondoka na ushindi.

“Katika mchezo wa leo (juzi), Liverpool ilipiga mashuti mangapi ambayo yalilenga lango? Nadhani yalikuwa mawili na waliweza kumiliki mpira kwa asilimia 65, lakini walishindwa kupata bao, hapo naweza kusema kuwa Liverpool walikuwa na tatizo.

“Ni wazi kwamba mchezo ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili, lakini nadhani tuliweza kuwamiliki wapinzani wetu, naweza kusema kuwa matokeo ya mchezo huo wala si mabaya kwa upande wetu, tunaangalia michezo ijayo,” alisema Mourinho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles