24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Kizimbani kwa kumnyonga mwanae

Mohamed Hamad

Jeshi la Polisi wilayani Kiteto Mkoani Manyara, limempandisha kizimbani mkazi wa Kijiji cha Partimbo wilayani humo, Paulina Peter (28) kwa tuhuma za kumnyonga mwanaye.

Mwendesha mashitaka wa Polisi, Vincent Kalege mbele ya  hakimu mkazi Kiteto amesema tukio hilo lilitokea usiku kijijini hapo baada ya mwanamke huyo kujifungua na kumnyonga mwanae kisha kumtelekeza mlangoni kwa mtalaka wake.

Mwendesha mashtaka huyo amesema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 199 kanuni ya adhabu sura namba 16.

Mtuhumiwa hakutakiwa kujibu kufuatia mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ambapo amedhaminiwa na watu watatu na kiasi cha Sh milioni 10 kwa pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles