31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

KIZIMBANI KWA KUBAKA MTOTO WA BOSI WAKE

 

STELLA SADOCK (DSJ) NA DOROTH MNUBI (TSJ), DAR ES SALAAM


MKAZI wa Tegeta Masait, Vitalis Joseph (24) ambaye ni mfanyakazi wa bustani , amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam akituhumiwa kumbaka mtoto wa bosi wake mwenye umri wa miaka tisa.

Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Caroline Kiliwa, Mwendesha Mashitaka, Ramadhani Mkimbu, alidai Novemba mwaka juzi na mwaka jana maeneo ya Tegeta Masait Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam alimbaka mtoto huyo wa miaka tisa (jina linahifadhiwa).

Mshitakiwa huyo alikana kutenda shitaka hilo ambapo Hakimu Kiliwa alisema dhamana yake ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wanaofanya kazi katika taasisi zinazo tambulika kisheria na dhamana ya maandishi ya Sh 500,000.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo na alirudishwa rumande hadi kesi yake itakapotajwa tena Agosti 15 mwaka huu.

Wakati huo huo mkazi wa Mwananyamala Kisiwani, Kondo Hamisi (25) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa shitaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa  Mwendasha Mashitaka, Ramadhani Mkimbu alidai mnamo Agosti mwaka jana huko Mwananyamala Kisiwani Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam uliiba Bajaji namba MC 923 BPT mali ya Zahra Seif na kumshambulia dereva kwa kumpiga panga.

Mshitakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo mbele ya Mahakama na Hakimu Kiliwa alisema upelelezi umekamilika na hana dhamana kwa shitaka lake hivyo kesi yake itasomwa tena Agosti 15 mwaka huu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles