28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kitwanga: nachafuliwa bila sababu

Charles Kitwanga
Charles Kitwanga

NA FREDRICK KATULANDA, MISUNGWI

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema wanaomhusisha na sakata la ufisadi wa Sh bilioni 37 linaloihusu Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited na Jeshi la Polisi, wana nia mbaya dhidi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jana Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Kitwanga alikiri kuwa mmoja wa waasisi na wamiliki wa Kampuni ya Infosys-IPS (T) Ltd iliyopewa kazi ya kufunga baadhi ya vifaa vya kutambua alama za vidole katika vituo vya polisi na Kampuni ya Dell kabla hajaingia katika siasa.

Hata hivyo, alisema baada ya kujiingiza katika masuala ya siasa, alimkabidhi mwanae Lunango Kitwanga, hisa alizokuwa akimiliki.

“Infosys walifunga vifaa vilivyonunuliwa na Kampuni ya Biometric ya Marekani kwa kampuni ya mawasiliano na kompyuta ya Dell ambayo ndiyo iliyowalipa.

“Kwa hiyo, wanaonihusisha na biashara hiyo wananichafua kwa nia mbaya.

“Lakini, awali nilikuwa na hisa asilimia 33 kwenye kampuni hii ya Infosys, lakini Agosti mwaka 2010, niliachia hisa hizo na sasa zinamilikiwa na mwanangu Lubango Kitwanga.

“Kwa hiyo, tangu hapo sikuwahi tena kuhusika na kampuni hiyo ingawa ukweli umekuwa ukipindishwa.

“Kwa kuwa nimesemwa mengi, nasema sasa imetosha, naomba mkafanye uchunguzi, mimi ni msomi, ninachukia sana uongo,” alisisitiza.

Wakati huo huo, Kitwanga alisema kwa sasa akili yake anaielekeza jimboni kwake kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles