23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kiti cha kuegemea ni kinga kising’olewe

bodabodaNa Kulwa Mzee -Dar es Salaam

BODABODA ni wafanyabiashara wakubwa wanaopaswa kuwezeshwa ili kukuza biashara yao lakini baadhi kwa bahati mbaya ama kwa makusudi hawajui thamani ya biashara wanayoifanya.

Kwanini nasema hivyo, hilo linaweza kuwa swali la baadhi ya watu lakini majibu yake ni ya wazi.

Pikipiki zinakuja zikiwa na muundo tofauti yote hayo ikiwa ni kuipendezesha mbele ya macho ya wateja.

Vyombo hivyo vya moto vipo vinavyokuja vikiwa na kiti nyuma kinachomwezesha mteja kuegama na nyingine kubwa haziko katika muundo huo nikimaanisha hakuna mahali pa kuegama.

Jambo la kushangaza ni pale kijana anapokabidhiwa pikipiki yenye kiti cha kuegemea anaamua kuingia kwa fundi ama mwenyewe hugeuka fundi na kuanza kufungua kiti.

Kiti kinafunguliwa kwa nia ya kumfaidisha dereva anayetamani kupakiwa mshkaki ili kupata fedha nyingine.

Dereva anaona akitumia kiti hicho anashindwa kupakia mshkaki na hata akilazimisha abiria wanaopanda wanatakiwa wawe wembamba.

Anaangalia hilo lakini anashindwa kujiongeza kuona kwamba pikipiki yenye kiti cha aina hiyo inaweza kuwa na wateja wengi hasa wazee ambao wanaegama kwa ajili ya kupata balansi.

Pamoja na wazee lakini wapo abiria ambao ni waoga wanapokuwa wakitumia usafiri huo hivyo inasaidia kutomuacha chini endapo kutatokea na dharura yoyote ikiwemo kuingia katika shimo ama michanga.

Vijana wanafanya biashara lakini hawajui wanamlenga mteja yupi, wao wakati wote wanawalenga vijana huku wakisahau kwamba wapo wazee na watoto wanaohitaji kupata huduma hiyo.

Mfanyabiashara anapoamua kufanya biashara anatakiwa kutoa huduma kwa wote bila kuwagawa katika makundi.

Hoja nyingine pamoja na kiti hicho kuwasaidia wazee na watoto kuwa huru wanakuwa safarini pia ni urembo wa chombo hicho.

Pikipiki yenye kiti cha kuegemea inapendeza kwa kuiangalia na kwa kupendeza huko inavutia kupata wateja wengi.

Ni ushauri kwamba si jambo la hekima kufanya uharibifu kwa kung’oa kiti cha kuegemea, thamini na kukijali chombo kinachokufanya uendelee kuishi.

Watengezaji waliamua kuweka kiti hicho wakiwa na maana kubwa, si tu kurembesha pikipiki lakini pia kulinda usalama wa abiria.

Tunapishana barabarani na bodaboda wakiwa wamepakia wanafunzi watatu lakini ulinzi wa hao watoto haupo kwani kila mmoja anashika shati la mwenzake ambalo kama ikitokea ajali linaweza kuchanika na wale wote wa nyuma wakaanguka.

Mtindo huo wa kushikana mashati unaweza kusaidia pale kiti kinapokuwa na mahali pa kuegamia.

Hivyo vising’olewe kwani hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo.

Acheni uharibifu wa vyombo vya moto vinavyowawezesha kuendesha maisha yenu na familia zenu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles