Kiongozi mbio za mwenge agoma kuzindua daraja kisa ujenzi haukuzingatia ushauri

0
668

Amina Omari, Handeni

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ally amegoma kuzindua mradi wa Daraja la Mfuto, lililopo katika eneo la Bwawani wilayani Handeni, kutokana na ujenzi wake kutozingatia ushauri wa kitaalamu.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi huyo ametoa  wiki mbili kwa Mhandisi wa Wilaya kuhakikisha anafanya upya vipimo vya mradi huo ili kuweza kujiridhisha na malighafi zilizotumika kama zina ubora.

Akiwa kwenye ziara ya mwenge huo katika kuzindua miradi mbalimbali, amesema miradi inayotekelezwa nchini inatokana na fedha za wananchi hivyo serikali haitakuwa tayari kuona fedha hizo zinatumika vibaya.

“Halmashauri hakikisheni hamumpi nafasi mkandarasi ya kujiamulia anavyotaka ni lazima kuhakikisha mnamsimamia ili aweze kujenga miradi katika viwango vyenye ubora,” amesema kiongozi huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here