Kylie Jenner akimbilia kwenye vinywaji

0
995

LOS ANGELES, MAREKANI

BAADA ya kufanya vizuri kwenye vifaa vya urembo, mwanamitindo kutoka familia ya Kardashian, Kylie Jenner anataka kuelekeza nguvu zake kwenye vinywaji vikali.

Kylie anatajwa kuwa tajiri namba moja kwa warembo wenye umri mdogo ambao wameweza kuwa na kipato kikubwa kutokana na biashara zao.

Mbali na kuwa tajiri namba moja, lakini bado hachoki kupambana na sasa ametangaza kuwa yupo njiani kuzindua vinywaji vyake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 21, amedai miongoni mwa vinywaji hivyo ni pamoja na mchanganyiko wa pombe kali, Wine, Spirits, liquor na vilevi vingine vingi.

Tangazo la uzinduzi wa vinywaji hivyo ameliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao unatajwa kuwa na wafuasi zaidi ya milioni 194.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here