23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kinyongo kinaua wanaume Iringa

FRANCIS GODWIN – IRINGA

TAASISI isiyo ya  kiserikali ya  Iringa  inayojishughulisha na masuala ya msaada  wa  kisheria  mkoani Iringa, Parelegal Centre (IPACE) imesema vifo vya baadhi ya  wanaume mkoani Iringa, vimekuwa vikisababishwa na  vinyongo  walivyonavyo   kwa  kufanyiwa  vitendo vya  ukatili  wa  kijinsia  kama  kupigwa na  wake zao na  kutunza siri  hiyo   moyoni.

Mwenyekiti  wa IPACE,   Issac  Kikoti  aliyasema hayo jana  wakati akizungumza na  waandishi  wa habari  kuhusu maadhimisho ya siku 16   za ukatili  wa  kijinsia Tanzania yanayofanyika kimkoa  Kijiji  cha Kiwere.

Kikoti alisema suala la  ukatili  wa kijinsia  ndani ya  mkoa huo ni kubwa pamoja na kuwa bado hakujawa na takwimu  sahihi.

Alisema  vitendo vya ukatili wa  kijinsia ni  miongoni mwa sababu  zinazochangia  vifo  kwa baadhi ya  wanaume,  hasa wale  ambao  wamekuwa  wakivumilia  mateso  ya  kupigwa na kutunza  siri hizo.

Kikoti alisema utunzaji wa siri  moyoni ni  miongoni  mwa  mambo yanayowatesa wanaume  na hata   kujikuta  wanapatwa na  vifo  vya ghafla.

“Wanaume   wengi  wananyanyasika   katika  ndoa zao,  wapo  ambao  wanapigwa na  wapo  ambao  wananyimwa  ‘ugali  wa  usiku’  na  wake  zao, ni  waoga wa  kutoka  nje  kwenda kulalamika  juu ya manyanyaso hayo na hii ni hatari  kukaa na  kitu  kibaya  moyoni,” alisema Kikoti.

Alisema  pamoja na matukio ya  ukatili  dhidi ya watoto kuwa makubwa  katika jamii, jamii  haipo  tayari  kujitokeza  kupinga  ukatili   huo.

Kikoti alisema suala la  kupinga ukatili wa  kijinsia  ni  jukumu la  kila mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles