24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Kinga za mabusha kutolewa nyumba za ibada, sokoni

VERONICA ROMWALD,  DAR ES SALAAM

WAKAZI wa Mkoa wa Dar es Salaam wenye umri wa kuanzia miaka mitano na kuendelea watapewa dawa kinga  dhidiya maambukizi ya matende na mabusha maarufu ‘ngirimaji’.

Dawa kinga hizo zitatolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia mpango wa taifa wa udhibiti wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa Taifa wa Mpango huo, Dk Upendo Mwingira alisema hilo litafanyika Desemba 15 hadi 20, mwaka huu.

Alisema zitatolewa bila malipo katika vituo vyote vya afya na hospitali zote za mkoa huo na maeneo maalum ambayo yatatengwa kama vile kwenye nyumba za ibada, sokoni na kwingineko.

“Matende na mabusha ama ngirimaji ni miongoni mwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

“Ugonjwa huu unaenezwa na mbu wa aina zote, ni muhimu mtu kukingwa kwani akiugua na akichelewa kupata matibabu kupona kwake ni vigumu,”alisema.

Dk. Mwingira alisema tangu mwaka 2009 Serikali ilianzisha mpango huo ambao manispaa 121 zilijumuishwa hadi kufikia sasamanispaa 93 sawa na asilimia 77 zimeweza kuukabili ugonjwa huo.

“Bado manispaa 28 ambazo zina kiwango cha juu, kwa upande wa mikoa ya Dar es Salaam na Lindi ndizo zenye kiwango cha juu zaidi.

“Tunaona katika Mkoa wa Dar es Salaam mwamko wa wananchi kujitokeza kumeza dawa kinga bado ni mdogo.

“Ndiyo maana tunawahamasisha wananchi kujitokeza kumeza dawa kinga hizi, matende na mabusha tunaweza kuyakinga mtu asipate kwa njia hii,”alisema.

Alisema hata hivyo mtu anapopata busha njia pekee ya kutibu ni upasuaji.

Alisema hadi wanaume 1,000 wamefanyiwa upasuaji wa kutibu mabusha na wengine 3,000 wanasubiri upasuaji.

Ugonjwa huo husababishwa na minyoo ambayo hubebwa na mbua napong’ata mwanadamu vimelea vya minyoo huingia mwilini mwake na kwenda kuzibanjia ya majimaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles