24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kufanya mazoezi holela ni hatari

 VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

MAZOEZI ni muhimu kwa afya ya mwanadamu lakini ikiwa yatafanyika holela muhusika anajiweka katika hatari zaidi badala ya faida, imefahamika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi alisema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalum.

Alisema kufanya mazoezi pasipo kuchunguzwa kwanza afya ni hatari kwa sababu  ikiwa mtu anakabiliwa na magojwa mbalimbali hususani ya moyo anaweza kuanguka na kufariki dunia ghafla.

“Ninapoona ‘wimbi’ la gym kila mahali huwa ninatafakari, je wale wanaokwenda huko kufanya mazoezi wamechunguzwa afya zao na nani?

“Nakumbuka katika gym (anaitaja) ni kubwa hapa Dar es Salaam, kuna mtu alianguka wakati akifanya mazoezi.

“Sasa hiyo ni gym kubwa na mtu alianguka, jiulize wangapi wanakwenda huko hawajijui afya zao.

“Ni hatari kama mtu ana shinikizo la damu anaweza kuanguka ghafla na kupoteza maisha au hata kupata kiharusi,” alisema.

  Dk Janabi alifafanua: “Kimsingi kadiri mtuanavyofanya mazoezi ndivyo mahitaji ya damu mwilini  mwake yanavyoongezeka, tunashauri mtu asifanye mazoezi ya aina yoyote hasa yale magumu na ya muda mrefu bila kuchunguza afya yake kwanza.

“Katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika Septemba 26, mwaka huu hapa JKCI tulitangaza upimaji afya bila malipo.

“Walijitokeza watu 801 kupima afya, watu 400 kati yao walikutwa wana shinikizo la juu la damu, 200 kati yao walikuwa hawajijui nakati ya 150 hadi 200 walikuwa wanajijua lakini walikuwa hawatumii dawa vile inavyopaswa na hivyo kuhatarisha maisha yao zaidi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles