KINANA AMLILIA WINNIE MANDELA

0
854

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania kutokana na kifo cha Mke wa zamani na Rais wa Afrika Kusini, Hayati Mzee Nelson Mandela, Mama Winnie Mandela aliyefariki Aprili 2, mwaka huu.

Mama Winnie Mandela ambaye pia ni Mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, amefariki jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 81. Mwanaharakati huyo anatarakiwa kuzikwa Aprili 14, mwaka huu.

Pamoja na viongozi wengine wa CCM, Kinana ameongozana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Gaudensia Kabaka, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI, Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi, Seif Shaban Mohamed na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here