22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

MBUNGE ADAI KUPAPASWA MAUNGONI

Fredy Azzah, Dodoma

Mbunge wa Kavuu, Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM), amedai kuwa walinzi wanaowakagua wakati wakiingia kwenye viwanja vya Bunge, wanawapapasa sehemu mbalimbali za miili yao.

Mbunge huyo amesema hayo leo wakati akiomba mwongozo wa kiti, jambo lililofanya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kupiga marufuku ukaguzi wa aina hiyo.

Amesema wanapopita kwenye mashine za ukaguzi hutakiwa kuvua mikanda, viatu, saa na vitu vingine na kwamba kibaya zaidi kwake ni suala la kupapaswa.

“Tunavua nguo, watu wanainua mashati kuvua mikanda na tunaona vitovu vya wanaume halafu miili inasisimka tukidhani wanataka kufanya maandalizi ya, mwili wa binadamu una vivutio vingi.

“Leo nimepita mashine moja vizuri na nilipofika ya pili ikalia. Nikaambiwa nikaguliwe sasa kibaya nakwenda kukaguliwa ananishikashika maeneo mbalimbali, hapa tuna mwezi mmoja huku si kutiana hanjamu,” amehoji.

Dk. Kikwembe amemtaka Spika kutoa agizo kukomesha jambo hilo, akisema halikubaliki na linawadhalilisha wabunge kila wakati.

Akijibu mwongozo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai ameagiza ukaguzi kwa kuwashika shika wabunge mwilini uachwe mara moja kwa kuwa unawadhalilisha na kuagiza utaratibu ufanyike kwa kuangalia namna bora ya kuwakagua wabunge kwani kinachofanyika ni ukaguzi wa kizamani uliopitwa na wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles