Kim Kardashian hataki kuongeza mtoto

0
704

LOS ANGELES, MAREKANI

MWANAMITINDO Kim Kardashian, ametangaza kusitisha kuongeza watoto katika familia yake huku akidai alionao wanatosha.

Awali alipokuwa na mtoto mmoja alitangaza nia ya kuwa na watoto wengi ili kuja kuwa na familia bora, lakini sasa ana jumla ya watoto wanne na amedai hafikirii kuongeza mwingine katika maisha yake.

“Nina nyumba ya watoto wanne nadhani hii inakamilika na hakuna sababu ya kuongeza mtoto mwingine, hawa wanatosha kuijenga familia bora,” alisema mrembo huyo mwenye umri wa miaka 38.

Mrembo huyo aliongeza kwa kusema, watoto wanne hatoshindwa kuwaleo hata kama atakuwa bize na mambo yake, ila zaidi ya hapo wanaweza kumpa shida.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here