Dully Sykes ahofia bifu

0
925

GLORY MLAY

MSANII mkongwe wa muziki wa bongo fleva, Dully Sykes, amesema anaogopa kutaja wasanii wakali kwa kuhofia kutengeneza bifu na wasanii wengine.

Dully amesema akianza kuwataja wasanii hao wengine watachukia kutokana na ukaribu alionao na kufanya kazi kwa muda mrefu.

“Kuna watu au wasanii ambao wapo kwa ajili ya mabifu hata kama hakuna anachofanya kwenye muziki, hivyo wanaofanya vizuri ni wengi ila nikianza kuwataja hapa utashangaa nanuniwa bila ya wengine kuwataja, nikipiga simu hazipokelewi.

“Hivyo ili kulikwepa hilo nawashauri tu waendelee kujituma kuhakikisha muziki hapa ndani unavuka mipaka unafika mbali, tuachane na mambo ya mabifu,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here