20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Kim Kardashian aguswa na shambulizi New Zealand

NEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian, amewataka viongozi nchini New Zealand kubadilisha sheria ya kumiliki silaha ili kuepuka matukio ya kigaidi.

Kauli hiyo ameitoa siku chache baada ya kutokea tukio la kigaidi huku watu 50 wakiuawa kwa kupigwa risasi na mtu aliyejitoa mhanga katika Mji wa Christchurch nchini humo.

“Ni wakati sahihi sasa kwa viongozi wa New Zealand kubadilisha sheria za kumiliki silaha, ikiwezekana kuzifungia kabisa baadhi ya silaha zisitumike kwa watu binafsi.

“Marekani imechukua hatua, kwanini viongozi wasifanye hivyo,” aliandika mrembo huyo na kuonekana kauli hiyo ikipewa sapoti kubwa na mashabiki mbalimbali, ikiwa pamoja na ndugu kutoka familia hiyo ya Kardashian.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles