24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Kilindi yaagizwa kukomesha migogoro

RC GeitaNa Amina Omari, Kilindi

SERIKALI mkoani Tanga imeliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi ya wilaya, kuhakikisha wanakomesha migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo imechangia kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Magalula Said Magalua wakati wa hafla ya kumsimika kiongozi mkuu wa wafugaji, Lweigwanani iliyofanyika katika Kijiji cha Elerai kilichopo Kata ya Kibrashi wilayani humo.

Alisema endapo viongozi hao watashirikiana kwa pamoja wataweza  kuzuia au kukomesha kabisa mapigano ya mara kwa mara ya wakulima na wafugaji ambayo yanasababisha  baadhi ya watu  kuuawa.

“Niwaombea pangeni timu za kuhakikisha mnashirikiana kati ya watendaji wa serikali, jeshi la polisi pamoja na hawa viongozi wa kimila ambao ndio wakuu wa jamii za wafugaji ili kutafuta namna bora ya kumaliza migogoro ya ardhi katika wilaya hii,” alisema RC Magalula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles