30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mabomu yarindima Kiteto Kura za maoni

NA BEATRICE MOSSES, MANYARA

JESHI la Polisi Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, limewatawanya wananchi wa eneo hilo kwa kutumia mabomu ya machozi, baada ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara kuvamiwa na wananchi.

Kabla ya vurugu kuibuka wananchi wa Kata ya Engusero walifunga barabara na kuwazuia wajumbe hao kufika Kiteto kuhakiki matokeo ya kura za maoni ya ubunge wa chama hicho.

Katika vurugu hizo wananchi hao walimvamia mbunge aliyemaliza muda wake, Benedict Ole Nangoro na kuwafanya polisi watumie mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kamati hiyo ya siasa, chini ya mwenyekiti wake, Lukas Ole Mukusi, akiwa na mjumbe aliyekuwa ameongozana nae, Christopher Ole Sendeka, walitokea Dodoma kwenda Kiteto kwa ajili ya kuhakiki matokeo ya nafasi ya ubunge.

Baada ya kufanyika uchaguzi wa kura za maoni kumpata mgombea wa CCM atakaepeperusha  bendera ya chama hicho, baadhi ya wagombea walikata rufaa kupinga matokeo.

Mgombea aliyepita katika kura za maoni Jimbo la Kiteto ni Emmanuel Papian, aliyemzidi mpinzani wake kwa kura 9,000, ambapo Ole Nangoro, alidaiwa kutoridhika na matokeo hayo.

Kwa mujibu wa wananchi hao, ujio wa kamati hiyo unalenga kubadilisha matokeo ambayo wanaamini aliyepatikana kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo hilo anafaa.

“Tunajua uteuzi wa mgombea huyo Papian umeleta manung’uniko kwa jamii ya kifugaji (wamasai), kwa madai kuwa maslahi yao hayatashughulikiwa na jamii nyingine”, alisema mwanachama mmoja.

Polisi wilayani Kiteto wamekiri kufungwa kwa barabara Kata ya Engusero kwa kuwekwa mawe barabarani, ili kuzuia msafara huo usipite kwenda Kiteto, wakidai kuwa wanaenda kubadilisha matokeo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles