22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Udhamini Ligi Kuu wapanda

Pg 32NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom, imeongeza udhamini wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa asilimia 40, kutoka shilingi bilioni 1.6 iliyopita hadi shilingi bilioni 2.3 kwa mwaka.

Vodacom ambao ni wadhamini wakuu wa ligi hiyo, jana imesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kuendelea kuusaidia mpira, mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 6.6.

Akizungumza jana katika hafla hiyo ya kusaini mkataba iliyofanyika Makao Makuu ya kampuni hiyo Mlimani City Dar es Salaam, Mkurugenzi Masoko wa kampuni hiyo, Kelvin Twissa, alisema wana furaha kuendelea kuwa sehemu ya udhamini wa ligi.

“Tunafurahia mafanikio ya timu bora na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa, hii inatokana na kuwa na ligi bora ambayo inadhaminiwa na Vodacom.

Twisa alisema fedha katika mkataba huo zimeongezwa katika maeneo machache, ambayo ni timu wakizingatia sana suala la usafiri wao kutoka kituo kimoja hadi kingine, gharama za waamuzi na wasimamizi wa mechi.

Alieleza kila timu italipwa shilingi milioni 800 kwa mwaka, ambapo malipo hayo yatafanyika kwa awamu nne, ikiwa na maana kila klabu itachukua shilingi milioni 200 kila baada ya miezi mitatu, huku akisisitiza hawatarajii kusikia malalamiko kutoka kwa klabu na wataanza kupewa fedha zao kabla ya kuanza ligi.

“Waamuzi wa Ligi Kuu Bara watalipwa shilingi milioni 60, wasimamizi wa mechi Sh milioni 63 na TFF shilingi milioni 183, wakati zawadi za washindi, mchezaji bora, kocha bora na

mwamuzi bora hazitaongezwa ambazo jumla yake ni shilingi milioni 174,” alisema.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, aliwashukuru Vodacom kwa kuwashika mkono huku akiwaomba wadhamini wengine kuwaunga mkono kwa kujitokeza.

“Tunawashukuru sana Vodacom, awali waliingia mkataba wa miaka mitano uliomalizika mwaka 2012, kipindi hicho ukiwa na thamani ya Sh milioni 300 kwa mwaka, ukaja udhamini wa miaka mitatu ambao thamani yake ilikua shilingi milioni 500, ukaja huu wa miaka mitatu tena ambao umemalizika juzi thamani yake ilikua shilingi milioni 800 kwa mwaka kabla wa leo tuliosaini ambao umeongezeka mara mbili, tunawashukuru sana,” alisema.

Rais huyo aliahidi kuangalia Fair Play katika ligi, ili kupata bingwa halali akieleza ipo siku atakuja kumkamata mwamuzi, mchezaji, viongozi ama klabu kwa ajili ya rushwa.

“Naendelea kuonya wanaotoa au kupokea rushwa tutawafukuza kwenye mpira maisha na kumfunga, haiwezekani watu wanatoka jasho uwanjani mwingine anakuwa tayari anajua matokeo,” alisema Malinzi.

Malinzi aliziasa klabu kuheshimu ushirikiano na mahusiano wanayoyapata kutoka Vodacom, kwani hawatafurahi kushirikiana nao kama kuna migogoro hivyo anaomba utulivu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles