30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Takataka zawawatisha wakazi Dodoma

NA PENDO MANGALA, DODOMA

WAKAZI wa maeneo ya Chang’ombe na Kizota katika Manispaa ya Dodoma, wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kuzagaa kwa takataka karibu na maeneo wanayoishi.
MTANZANIA imebaini kuwapo kwa takataka hizo katika maeneo hayo ambazo zimesababisha mazingira hayo kuwa katika hatari ya kuambukiza magonjwa na kuwa tishio kwa wakazi wanaoendesha shughuli zao katika eneo hilo.
Mmoja wa wakazi wa Chang’ombe ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema taka hizo zimekuwa zikitupwa na watu ambao si
wakazi wa maeneo hayo jambo ambalo limekuwa kero kwao.
“Kiukweli kuna baadhi ya watu ambao hawajui maana ya usafi, na kwamba
humwaga taka hizo wakati wa usiku na kutusababishia usumbufu mkubwa.

“Ni vyema sasa manispaa ikachukua hatua stahiki za kutekeleza sheria ndogo ndogo za usafi kwani suala la taka katika mazingira tunayoishi ni hatari kwa afya zetu,” alisema mkazi huyo.
Baadhi ya wananchi walitaka kuwapo na adhabu kwa wakazi watakaobainika kutupa taka ovyo ili kudhibiti tabia hiyo.
Gazeti hili liliwatafuta maofisa afya wa Manispaa ya Dodoma kwa njia ya simu za mkononi ili kuzungumzia suala hilo, lakini hawakuweza kupatikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles