22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi Morogoro kuchaguana Agosti 22

Na Ashura Kazinja, Morogoro

HEKAHEKA ya kupata viongozi wapya  watakaoongoza kwa miaka mitatu Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro (MOROPC) zimeanza.

Hayo yalibainishwa na mratibu wa klabu hiyo, Thadei Hafigwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa ambapo alisema uchaguzi huo utafanyika Agosti 22, mwaka huu.

Alisema uchaguzi huo unafanyika ili kutekeleza azimio la mkutano mkuu wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ili kuiweka vema kalenda ya umoja huo na kuuwezesha kuweka upya bodi yake.

“Hivi tunavyoongea baadhi ya klabu nchini zikiwamo za mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Simiyu, Tabora, Dodoma na Pwani zimeshatekeleza azimio hilo kwa kuchagua viongozi wao.

“Nasi tumeshaanza mchakato kutekeleza azimio hilo ambapo kamati tendaji katika kikao chake imebariki mkutano mkuu maalumu ufanyike Agosti 22, mwaka huu,” alisema Hafigwa.

Kwa mujibu wa mratibu huyo, nafasi zitakazogombewa ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti na makamu wake, katibu na msaidizi wake, mweka hazina na msaidizi wake na wajumbe watano wa kamati tendaji.

Alisema gharama za fomu ni Sh 20,000 na 15,000 kulingana na nafasi inayoombwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles