24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kijana wa kazi adaiwa kuua watoto wa familia moja

 GUSTAPHU HAULE – PWANI 

WATOTO wawili wa familia moja wameuawa na kijana wa kazi za ndani na yeye kuuawa na wananchi waliokuwa na silaha mbalimbali za jadi katika Kijiji cha Kwazoka, Chalinze mkoani Pwani. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa moja usiku katika Kijiji cha Kwazoka, Wilaya ya Kipolisi Chalinze mkoani Pwani. 

Alisema Yasin Abdallah (35) mfanyakazi wa ndani wa Wema Senzie, aliwaua watoto wawili kwa kuwakata na mapanga na kumjeruhi mama yao Saada Salehe (28). 

Kamanda Nyigesa aliwataja watoto waliouawa kuwa ni Rehema Makolo (5), mwanafunzi wa shule ya awali na Abubakar Makolo (6) darasa la kwanza ambao wote walikuwa wanasoma Shule ya Msingi Kwazoka. 

Alisema baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo la mauaji, wananchi walimkamata na kumuhifadhi katika ofisi ya kijiji na kwamba akiwa humo alivunja mlango na kukimbia, lakini wananchi walifanikiwa kumkamata na kumshambulia kwa silaha za jadi hadi kufariki dunia. Kamanda Nyigesa alisema majeruhi ambaye ni mama wa watoto hao, amelazwa Kituo cha Afya Mlandizi akipatiwa matibabu huku maiti zikihifadhiwa katika kituo hicho kusubiri taratibu za mazishi. 

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na kwamba taarifa za awali za kiuchunguzi kuhusiana na mauaji hayo zinaeleza kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya mama wa watoto hao na kijana huyo wa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles