25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Kijana aliyechana Quran akamatwa

Ashura Kazinja, Morogoro

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kukamatwa kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Maleki (30), kwa kosa la kuchana na kuchoma moto kitabu cha Juzuu Amma ambacho ni sehemu ya Quran Tukufu.

Video ya kijana huyo akichana kitabu hicho imeonekana kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, kitendo ambacho kimeonekana kuwagusa na kuwachukiza watu wa kada na dini tofauti ambapo wamekemea kitendo hicho na kutaka kijana huyo achukuliwe hatua.

Amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano Februari 6, saa nane mchana katika eneo la Uhindini mkoani Morogoro.

“Maleki ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Mbumi ‘B’ Kilosa na pia Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, alionekana akiwa anachana na kuchoma kitabu hicho Kitakatifu cha dini ya Kiislamu.

“Kitendo ambacho kiliwakasirisha waumini wa dini hiyo na wananchi waliokuwa maeneo hayo na kuamua kutoa taarifa kwa jeshi la polisi Wilayani Kilosa,” amesema Kamanda Mutafungwa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles