Mtitu: Natamani Lulu Diva aache muziki

0
1392

Glory Mlay

MSANII na mtayarishaji wa filamu maarufu nchini, William Mtitu, amesema anatamani Lulu Diva aache muziki awekeze nguvu zake kwenye filamu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mtitu alisema anaamini Lulu Diva anakipaji cha kuigiza kuliko kufanya muziki na angepata mafanikio makubwa kuliko alivyo sasa.

“Ukinuliza nitakwambia natamani Lulu Diva aache muziki, akiwekeza nguvu kwenye filamu atafika mbali maana alijaribu tu kwenye Rebeca na alifanya vizuri ,waigizaji wengi wa kike huwa wanakuja alafu baadae wanaacha.

“Naamini angeendelea kuigiza angekuwa anga za kimataifa, anakipaji lakini amekificha kwenye muziki,” alisema Mtitu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here