24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kibao kipya cha Mr Eazi; Personal Baby

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

STAA wa Muziki kutoka nchini Nigeria, Oluwatosin Ajibade maarufu kama Mr Eazi ameachia ngoma yake mpya, Personal Baby ambayo ni ya pili kuachiwa kutoka katika albamu yake mpya ambayo bado hajaiachia.

Wimbo huo umetengenezwa na  Prodyuza Kel P ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Grammy, akiwa amewahi kufanya kazi na mastaa wakubwa nchini humo kama Burna Boy, Wizkid na Angelique Kidjo.

Kwa upande wa video, amesimama Muongozaji(Director) maarufu, Ademola Falomo ambaye amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha vionjo vya muziki wa asili wa Banku alivyoviweka Mr Eazi katika wimbo huo, vinaendana na video husika.

Kwa upande wa uandishi, Mr Eazi ameshirikiana kuandika na msanii mwenzake, Teni ambapo mashairi yake yanazungumzia zaidi mapenzi, ukiwa ni wimbo wa pili baada ya Legalize.

Legalize unaendelea kufanya vizuri kutoka kwa msanii huyo na unaweza kuisikiliza au kuitazama kwenye majukwaa yote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles