25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Kehlani akimbizwa hospitali baada ya kunywa sumu

Kehlani ParrishNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Kehlani Parrish, amekimbizwa hospitali baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujiua.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 20, alifikia hatua hiyo kutokana na baadhi ya watu kudai kwamba ni msichana mbaya katika mapenzi.

Inadaiwa kwamba mrembo huyo ana tabia mbaya kwa wanaume anaotoka nao kimapenzi kutokana na kutodumu nao na huwa akiwaacha wakiwa katika mazingira magumu.

Lakini hali ya msanii huyo kwa sasa inaendelea vizuri na ameweka ujumbe kupitia akaunti yake ya Instagram huku akiwa hospitali na kuandika: “Niliamua kuchukua hatua hii baada ya kusemwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kuwa sio mwanamke mzuri.

“Niliona bora nipoteze maisha yangu kuliko kuishi katika dunia hii ambayo ina kila aina ya majungu hasa pale ninapokuwa na mwanaume mpya, ila kwa sasa naendelea vizuri japokuwa nipo hospitalini,” aliandika Kehlani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles