30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Kauli yamponza Jose Mourinho

Jose MourinhoLONDON, ENGLAND

CHAMA cha Soka England (FA), kimemfungia mchezo mmoja kuingia uwanjani na faini ya pauni 50,000 kocha wa timu ya Chelsea, Jose Mourinho.

Adhabu hiyo imekuja baada ya kocha huyo kukutwa na kosa la kuvunja kanuni za FA inayohusiana na maelezo yake ya mwisho wa mchezo walipofungwa na Southampton mabao 3-1.

Mourinho alikutwa na kosa la kumbwatukia mwamuzi wa mchezo huo, akidai kuwa aliwaua baada ya kuwa na ‘hofu ya kutoa maamuzi kwa Chelsea’.

FA imesema kuwa ina uwezo wa kukatiwa rufaa kama hataweza kupatikana na kosa hilo tena kabla ya Oktoba 13 mwakani 2016 kwa kuvunja kanuni kupitia maneno yanayohusiana na hayo au kupitia vyombo vya habari.

Hiyo ni adhabu ya nne kwa Mourinho tangu arejee kwenye Ligi Kuu England mwaka juzi na faini alizolipa mpaka sasa zinafikia pauni 93,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles