Peter Manyika atoa ‘single’ ya tatu

0
1290

Manyika PeterNA MWANDISHI WETU

KOCHA wa makipa wa Timu ya Taifa, Peter Manyika, ameachia wimbo wa tatu aliouita ‘Karudi Baba Mmoja’ akinukuu vitabu vya zamani vilivyokuwa vikifundishiwa shuleni.

Wimbo huo wenye mahadhi ya Zouk ameimba kwa ustadi mkubwa akieleza kisa kizima cha baba huyo aliyerudi toka safari ya mbali aliyewataka watoto wake wakitaka urithi wataupata shambani.

“Niliamua kuimba kwa mafunzo, lengo likiwa ni kuwataka vijana wafanye kazi wasifikirie mali za kure bure badala ya kufanya kazi, ikiwemo kilimo ambacho wengi hukikimbia,’’ alisema Manyika, ambaye mtoto wake ni kipa wa timu ya Simba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here