29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Kumbe Martial aliitosa Chelsea

Anthony MartialMANCHESTER, ENGLAND

KLABU ya Chelsea inadaiwa ilitoa ofa nono zaidi ya Manchester United ili kumsajili kinda Anthony Martial, taarifa kutoka Ufaransa zimeeleza juzi.

Jarida la CanalPlus limesema kuwa straika huyo wa zamani wa Monaco aliipiga chini ofa ya The Blues kwa kuwa alikuwa na ndoto ya kuhamia United, ambayo ilikamilisha usajili wake kwa pauni milioni 36.

“Kwa mujibu wa taarifa zetu, Chelsea ilipanga kutoa fedha nyingi zaidi ya Manchester United kwa ajili ya Anthony Martial, lakini mchezaji mwenyewe alikuwa na ndoto ya kucheza Red Devils,” lilieleza jarida hilo.

Martial, aliyesajiliwa Septemba Mosi kwa ada itakayopanda na kufikia pauni milioni 58, amefanya makubwa uwanjani tangu ajiunge na miamba hiyo ya Old Trafford.

Mfaransa huyo, 19, amefunga mabao manne kwenye mechi saba alizocheza kwa mashetani hao wekundu, alianza kuwavutia mashabiki dakika chache alipofunga bao katika mechi yake ya kwanza walipocheza na mahasimu wao, Liverpool.

Kocha Mkuu wa United, Louis van Gaal, alipambana na matajiri hao na kumnasa Martial, licha ya rekodi zake kuonyesha alifunga mabao 13 tu Monaco.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles