23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kanye West anawaza kumtoa Trump Ikulu

kanye-west

Na BADI MCHOMOLO

NI wiki moja sasa tangu Marekani wafanikiwe kumpata Rais Mteule, Donald Trump, ambaye atakuja kuiongoza nchini hiyo hadi uchaguzi wa mwaka 2020.

Ifikapo 2020 utafanyika uchaguzi mwingine wa kumtafuta Rais ambaye atafaa kuiongoza nchini hiyo kwa miaka mingine minne.

Kama Wamarekani wataridhika na mwenendo wa Rais huyo  basi wanaweza kumpa nafasi ya kuendelea kuwa rais, lakini kama watakuwa tofauti nayo basi hawawezi kumpa nafasi hiyo kwa mara ya pili.

Trump ni mfanyabiashara maarufu nchini humo lakini amefanikiwa kutimiza ndoto za kuwa Rais wa nchi hiyo.

Rais huyo anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 3.7 kwa mujibu wa mtandao wa Forbes. Ni wazi kama atamaliza miaka minne basi atapambana kuhakikisha anaongeza minne mingine.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na ushindani katika kuwania nafasi hiyo dhidi ya mke wa Barack Obama, Michelle Obama na rapa maarufu nchini humo Kanye West.

Rapa Jay Z ni miongoni mwa wasanii wanaotamani kuona Michelle akiwania nafasi hiyo mara baada ya Hillary Clinton kushindwa dhidi ya Trump, lakini hadi sasa Michelle hajasema kama atakuja kuwania nafasi hiyo 2020, lakini Kanye West ameweka wazi hilo.

Septemba 2015, Kanye West aliweka wazi nia ya kutaka kuwania kiti cha urais ifikapo 2020 na hakutaka mwaka huu kwa kuwa aliamini kuwa hawezi kufanikiwa kutokana na maandalizi kuwa madogo.

Kutokana na hali hiyo amedai anataka kufanya maandalizi ya nguvu kwa ajili ya kushindana na mpinzani wake, hivyo maandalizi hayo tayari ameyaanza tangu mwaka jana mwishoni.

Kitu ambacho anakiamini msanii huyo kuwa anaweza kushinda urais ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Instagram na Facebook.

Msanii huyo ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola milioni 145, akiwa hajafikia hata nusu ya Trump, lakini anachokiamini ni idadi kubwa ya marafiki katika mitandao ya kijamii.

Kanye amedai hata bila ya kujali kuwa hana uzoefu kwenye masuala ya siasa, lakini kutokana na umaarufu wake anaweza kuwa msanii wa kwanza kuingia Ikulu ya Marekani.

“Wakati ninatoa wazo la kutaka kuwania urais mwaka 2020 sikuwa na maana kuwa nina mtazamo katika siasa, lakini nina mtazamo katika ubinadamu na ukweli kwa kila mtu.

“Ninaamini nina nafasi kubwa ya kushinda nafasi hii kutokana na idadi kubwa ya marafiki ambao niko nayo kwenye mitandao ya kijamii, najua kwamba sio wote ambao wanaishi nchini Marekani, lakini wengi wao wapo hapa na wananikubali.

“Kutokana na hali hiyo naweza kusema kuwa sina wasiwasi na nafasi hiyo. Wengi hawakuamini kama Trump anaweza kuwa Rais, lakini sasa ni Rais, hivyo ninaamini wengi hawaamini kama nitaweza kushinda kiti hicho ila naanini chochote kinaweza kutokea,” alisema Kanye.

Msanii huyo mwaka huu amekuwa akizungumziwa sana kutokana na aina ya video zake za kudhalilisha watu maarufu.

Video yake ya Famous ambayo inamwonesha Chris Brown, Trump, Kim Kardashian, Ray J, Amber Rose, Rihanna na wengine wengi wakiwa utupu ilizidi kumpa jina mwaka huu japokuwa aligombana na baadhi ya watu hao.

Mwenyewe anadai kuwa, kugombea urais nchini Marekani sio lazima uwe mwanasiasa au uwe mjuaji sana wa siasa kama ilivyo kwenye nchi nyingine.

Ana ubavu wa kumng’oa Trump? Ni mapema sana kujua hilo, lakini tumuache na ndoto zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles