24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Kane nje hadi mwisho wa msimu

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amethibitisha kuwa timu hiyo itaikosa huduma ya mshambuliaji wake, Harry Kane ambaye aliumia enka juzi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City.

Katika mchezo huo ambapo Tottenham walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika hatua hiyo ya robo fainali ya kwanza, lakini mchezaji huyo hakuweza kumaliza dakika 90 na kujikuta akitolewa nje dakika ya 55 baada ya kuchezewa vibaya na Fabian Delph.

Kane alitoka nje huku akiwa anatembea kwa kusaidiwa kwa kuwa mguu wake wa kushoto alikuwa hawezi kukanyaga chini kutokana na tatizo hilo. Hata hivyo, nafasi yake ikachukuliwa na Lucas Moura, huku dakika ya 78 Son Heung-Min akaiandikia bao timu hiyo.

Mbali na ushindi huo, kocha wa timu hiyo ameweka wazi kuwa, mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa Kane msimu huu.

“Ni jambo la kuhuzunisha. Mchezo wa marudiano utakwenda kuwa mgumu dhidi ya Manchester City huku tukimkosa mshambuliaji wetu Kane, ninaamini atakuwa nje hadi mwisho wa msimu,” alisema Pochettino.

Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa mchezaji huyo raia wa nchini England kuumia enka kwenye mguu huo, alipata tatizo hilo Januari 13, mwaka huu na kumfanya awe nje ya uwanja kwa wiki sita.

Kutokana na tatizo hilo, inaonekana kuwa mchezaji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki sita, wakati huo Tottenham ikiwa imebakisha michezo sita kumaliza michuano ya Ligi Kuu.

Kane mwenye umri wa miaka 25, hadi kufikia sasa amecheza jumla ya michezo 38 msimu huu kwenye michuano mbalimbali na kufanikiwa kupachika mabao 24.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles