24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kamwelwe ataka utaratibu abiria ndani ya daladala kukabili corona

RAMADHAN HASSAN – DODOMA

KUTOKANA na ugonjwa wa corona kuingia nchini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imetoa siku tatu kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) kukutana na halmashauri za majiji na miji kuweka utaratibu utakaodhibiti wingi wa watu katika vituo vya mabasi na idadi ya watu wanaotakiwa kusimama ndani ya daladala.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana, Waziri wa wizara hiyo, Isack Kamwelwe alisema hatuia hiyo imekuja kwa kuzingatia maelekezo ya rais pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuhusu kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo.

 “Ninaagiza Latra ndani ya siku tatu kukutana na halmashauri za majiji na miji kuweka utaratibu utakaodhibiti wingi wa watu katika vituo vya mabasi ya masafa marefu.

“Wamiliki, madereva, makondakta na abiria wa mabasi wahakikishe wanatumia vitakasa mikono mara kwa mara, baada ya kushika nyaraka au maeneo yanayoweza kuhifadhi virusi vya corona,” alisema Kamwelwe.

Pia aliagiza kampuni za mabasi kuangalia uwezekano wa kuwa na vituo vingi maeneo mbalimbali ya mijini ya kukatia tiketi ili kupunguza msongamano katika vituo vikuu vya mabasi.

Alisema Serikali ipo hatua za mwisho kukamilisha mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya kieletroniki ambao utapunguza kwa kiwango kikubwa mikusanyiko ya watu katika vituo vya kukatia tiketi.

“Tunashauri abiria wa mabasi ya masafa marefu wasisindikizwe na watu wengi ili kupunguza msongamano katika vituo vya mabasi.

“Ninaiagiza Latra kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Afya na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na wadau ndani ya siku tatu washauri idadi ya watu watakaoruhusiwa kusimama katika daladala,” alisema.

Pia aliagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), wahakikishe kunakuwa na vitakasa mikono vya kutosha katika maeneo ya bandari na katika viwanja vya ndege.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles