29 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Silent Ocean yatimiza miaka 17 ya utoaji huduma

Beatrice Kaiza, Dar es Salaam

Kampuni ya Wafanyabiashara ya ‘Silent Ocean’ imesheheherekea kutimiza miaka 17 tangu ianze kutoa huduma hafla iliyoenda sambamba na futari katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abukabar Kunenge ambaye alikuwa ni miongoni mwa viongozi walioshiriki kwenye shughuli hiyo ya kutimiza miaka 17 tangu ilipoanzishwa kampuni hiyo ya usafirishaji.

Aliipongeza kampuni hiyo kea hatua kubwa iliyopiga huku akiihakikishia kuwa Serikali iko sambamba katika kuhakikisha kuwa inaendelea kufanya vizuri.

“Nishukuru sana walioandaa shughuli hii ni tukio adimu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani, nilitakiwa kuwa airport kumpokea Waziri Mkuu, nilipomwambia kuhusu shughuli hii alinipa ruhusa nije kuhudhuria na kuniambia niwape salamu ya kwamba serikali ipo pamoja nanyi.

“Mimi ndio Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ndio Mwenyekiti wa kamati ya mapato ya Mkoa ndio Mwenyekiti wa kamati ya Usalama na Ulinzi ya Mkoa, Mwakilishi wa Rais katika Mkoa huu nawatamkieni fanyeni biashara sisi wajibu wetu ni kutatua kero zenu.

“Nyie ni kitovu cha biashara kama zamani baada ya serikali kuendelea kuondoa changamoto mbalimbali ambazo zilifanya biashara nyingi kusuasua na kupoteza masoko ya nchi jirani ambazo zilikuwa zinalitegemea soko hilo,” amesema Kunenge.

Kwa upande wake Mkurugezi wa kampuni, Mohamed Soloka, amesema kuwa ‘Silent Ocean ni kampuni ya wafanyabiashara yenye lengo la kuwasaidia kufikisha malengo yao kibiashara kukuza mitaji yao.

“Tunawashukuru wote kwa kuweza kufika na kuwa sehemu ya waliotuwezesha kufurahi pamoja katika kuadhimisha miaka 17 ya huduma ulikuwa ni wa umuhimu hatunabudi kuendelea kuwashukuru na tunaomba kuendelea kutupa ushirikiano wa dhati ili tuendelee kuwapatia huduma bora,”amesema Soloka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,212FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles