24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kidato cha sita, Ualimu kuanza mitihani ya kuhitimu kesho

Jeremia Ernest, Dar es Salaam

Jumla ya watainiwa 90,025 wa kidato cha sita kesho Mei 3, wanatarajiwa kuanza mtihani wa kitaifa wa kuhitimu kidato cha sita pamoja na mitihani ya Ualimi.

Akitoa ratiba hiyo leo Jumapili Mei 2, 2021 jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza Mitihani la Tanzania (NECT), Dk. Charles Msonde amesema mtihani huo unatarajiwa kufanyika kwenye shule 804 za Sekondari ambapo watahiniwa wa kujitegemea ni 248 na vyuo vya Ualimu 75 Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema kati ya watainiwa hao, washule ni wavulana 46,233 sawa na asilimia 56.84 na wasichana ni 35,110 sawa na asilimia 43.16.

“Mitihani hii inanza kesha Mei 3 hadi 25, mwaka huu, aidha watahiniwa wenyewe mahitaji maalum wapo 118 kati yao 95 ni wenye uoni hafifu na 23 ni wasiooona,” amesema Dk. Msonde.

Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea 8,682 waliosajiliwa, wanaume ni 5,759 sawa na asilimia 66.33, wanawake 2,923 sawa na asilimia 33.67 kati ya hao mtahiniwa asiyeona ni mmoja.

Ualimu

Amesema watahiniwa 6,973 waliosajiliwa kufanya mitihani ya kozi za Ualimu kati yao 2,187 ni ngazi ya Stashahada na 4,786 ni ngazi ya cheti ambapo watahiniwa wa Stashahada ni 1,446 sawa na asilimia 66.12.

“Kwa upande wa ngazi ya cheti watahiniwa ni 4,786, waliosajiliwa ni 2,637 sawa na asilimia 55.10, watahiniwa wa ngazi ya cheti wenye uoni hafifu ni 3 na wasioona 2,” amesema Dk. Msonde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles