25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 6, 2022

Contact us: [email protected]

Kampuni ya SBC yahimiza wengine kusaidia watoto wenye mahitaji maalum

zinga-pix-1 zinga-pix-2

Kampuni ya vinywaji baridi ya SBC Tanzania Limited  (Pepsi) imetoa msaada kwa  watoto yatima 38 wanaolelewa kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Amani kilichopo Zinga,  Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Roselyne Kwelukilwa, wameona ni vyema kuisadia na kuiunga mkono Serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu.

“Kampuni ya Pepsi imekuwa mstari wa mbele wa kusaidia jamii kwa kuhakikisha watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu wanapata elimu na huduma nyingine za msingi”, alisema Kwelukilwa.

Aliongeza kuwa, ” Watoto wanahitaji upendo, haki ya kupata elimu bora na kushiriki  kwenye michezo ili kuwa na afya njema na kuboresha uelewa  darasani,” ameendelea kusema Kwelukilwa.

Pepsi kwa kushirikiana na wateja wao, Spurs, ambao wanaendesha migahawa ya chakula katika zaidi ya nchi 15 duniani, ilitoa vifaa na msaada mbali mbali ikiwemo kilo 300 za mchele, nguo, vifaa vya elimu, vitabu, viatu, meza ya kuchezea mpira (soccer table) na vikaragosi (toys) .

Naye Lokesh Marakala, Meneja Uendeshaji wa Spurs amesema kuwa wanashirikiana na wadau wao, wakiwemo kampuni ya Pepsi kusaidia jamii, ndio maana kila mwezi wanatoa msaada kwa vituo vitatu vya watoto watima.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho, Margareth Mwegalawa aliishukuru kampuni ya SBC Tanzania Limited  (Pepsi) na Spurs kwa msaada wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,606FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles