27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Kampala Inter yaipigia hesabu Kinondoni UTD Ndondo Cup

Na Victoria Godfrey, Mtanzania Digital

Kocha Mkuu wa timu ya Kampala Inter Joseph Marwa, amesema wamejipanga kufanya vizuri ili kupata matokeo mazuri dhidi ya Kinondoni UTD katika mchezo wa Ndondo Cup utakaochezwa Julai 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kinesi Dar es Salaam..

Kampala ilianza kwa kishindo kwa kuibuka na ushindi wa mabao kuibuka na ushindi wa mabao 3_1 dhidi ya majohe UTD katika mchezo wa hatua ya 32 bora uliochezwa Jumatatu ya wiki hii kwenye Dimba la Bandari Temeke, Dar Es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA Digital Marwa, amesema pamoja na ushindi huo kasoro ameziona kasoro anakwenda kuzifanyia kazi kqbla ya mchezo huo.

Amesema malengo ni kuahakikisha wanavuna pointi tatu za mchezo ujao ili kujitengenezea njia ya kufuzu hatua ya 16 bora.

“Hatua hii kila timu inachezwa mechi tatu,hivyo tayari tuna pointi tatu na sasa tunapigana tupate tatau za mchezo ujao ili tutimize malengo ya kufuzu hatua 16 bora,” amesema Marwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles