23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

KAMATI YA BUNGE YASHINDWA KUWASILISHA TAARIFA YA USALAMA

Na MAREGESI PAUL-DODOMA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama imeshindwa kuwasilisha bungeni taarifa yake iliyopatikana baada ya kukutana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Taarifa hiyo ilitolewa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Adadi Rajabu, alipozungumzia ufanyaji kazi wa kamati hiyo, iliyotarajia kuwasilisha ripoti yake bungeni jana.

“Ni kweli Mheshimiwa Naibu Spika, Septemba 8, mwaka huu, Spika aliagiza kamati yangu itafakari hoja za Mheshimiwa Hussein Bashe kuhusu usalama wa Taifa na tukatakiwa tukutane na vyombo vya ulinzi na usalama ili baadaye taarifa yetu tuiwasilishe leo (jana) hapa bungeni.

“Lakini kutokana na unyeti na umuhimu wa jambo lenyewe, taarifa yetu tumeshindwa kuikamilisha. Kwa hiyo, tunaomba tuendelee kuifanyia kazi kesho na nakuahidi tutaikamilisha kabla hatujasambaratika hapa na kuiwasilisha kwako,” alisema Adadi.

Kutokana na taarifa hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alimtaka Adadi aandike barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, kumtaarifu jinsi kamati yake inavyohitaji muda zaidi ili wabunge watangaziwe juu ya mabadiliko hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles