25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge yakagua  mradi wa umeme Kinyerezi

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, imefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya mradi wa umeme Kinyerezi 1, utakaotumika katika reli ya kisasa ya SGR ambapo imefurahishwa na maendeleo yake.

Akizungumza leo Desemba 13,2023 jijini Dar es Salaam baada ya ukaguzi wa kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema ziara hiyo iliyoanzia Morogoro imefikia tamati.

“Kamati hii imetushauri mambo kadhaa ikiwemo kuongeza na kuchagiza mambo yanayoweza kuboresha uchumi wa wananchi, mfano kuwekeza kwenye gesi inayotumika kwenye magari,” amesema Kapinga.

Naye Mwenyekiti wa hiyo,  Daniel Sillo ambaye ni Mbunge wa Babati vijijini amesema Watanzania wana hamu ya kuona safari za reli ya SGR zinaanza, hivyo lengo la ziara yao ni kuona maendeleo na hatua zilipofikia.

“Kamati tumekuja kushuhudia kazi inayofanyika katika chanzo cha umeme unapozalishwa, tumeona Lot 1 (Awamu ya SGR) ya Dar es Salaam hadi Moro imekamilika kwa 100% ikitimua gharama ya bilioni 76.23, eneo linalofuata kutoka Morogoro hadi Dodoma kiasi kilichotumika ni bilioni 97.75 na imefikia 99%, tunaipongeza Serikali kwa hatua hii.” amesema Sillo.

Amesema kwa ujumla  miundombinu yote imekamilika  kwa asilimia kubwa na tayari kwa kuanza kazi .

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, amesema wizara hiyo  kupitia Shirikisha la Umeme Tanzania (TANESCO) imejiandaa kwa ajili ya mradi wa SGR na ziara hiyo ambayo pia ilihusisha eneo la Msamvu (Morogoro) kabla ya kufika Kinyerezi inalenga kubaini maendeleo ya kazi zilipofikia.

 “Kamati imeridhika na kazi ambayo imefanyika, ziara hii pia imetembelea GASCO ambao ni wasambazaji wa nishati ya gesi kwa ajili ya uzalishaji, wametoa maelekezo ambayo tumeyachukua,” amesema Mbuttuka.

Amesema kuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere litakapoanza uzalishaji wa umeme Januari  mwaka 2024 litaweza kupunguza matumizi ya gesi ambayo itahamishiwa kwenye matumizi ya viwandani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Petroli Tanzania  (TPDC), Mussa Mohammed Makame amesema wanafahamu kuna changamoto ya foleni kwa wenye magari wanaotumia nishati ya gesi, lakini Serikali inafanya inaendelea kuboresha huduma ya nishati ya gesi ili iwe ma mazingira rafiki.

“Wizara kupitia TPDC tayari wana mkakati huu, wana vituo vitatu na tunajenga vituo vitatu vingine, tumeingia ubia na sekta binafsi kwa ajili ya uendelezaji wa kujenga vituo vingi zaidi ili wananchi wapate moyo wa kubadilisha mfumo wa magari yao kuwa ya matumizi ya gesi kwa kuwa watakuwa wanapata gesi kwa wepesi zaidi, “amesema Makame.

Pia Kamati hiyo  imewashauri taasisi ambazo zina watu zaidi ya 100 waendelee kufungiwa gesi kwenye taasisi zao, hilo wamelipokea na wanalifanyia kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles