23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

KAMANDA MULIRO APATA KICHEKESHO KUPORWA MHASIBU ST. ANNE MARIA

Na AGATHA CHARLES                 |            


TUKIO la kuporwa fedha kiasi cha Sh milioni 3.5 alizokuwa amebeba Mhasibu wa Shule ya St. Anne Maria iliyoko Mbezi, Dar es Salaam, limemwachia maswali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro.

Akizungumza kwa simu na MTANZANIA Jumapili jana, Kamanda Muliro, alisema mazingira ya mhasibu huyo kuporwa ndiyo yanasababisha mlolongo wa maswali.

Alisema mhasibu huyo alitoa maelezo kuwa kabla kuporwa aliandamana kwenda benki na mwalimu wa shule hiyo ambaye alimpa namba za siri (password) ili amtolee fedha hizo.

Kamanda Muliro alisema mhasibu huyo alidai kuwa aliporwa fedha hizo akiwa geti la kuingilia shule hiyo baada ya kutoka benki.

Alisema licha ya kisa hicho kuchunguzwa, lakini moja ya maswali anayojiuliza ni kwanini mhasibu huyo hakuchukua polisi wakati wa kwenda kutoa fedha hizo benki kama ilivyo kawaida yake.

“Siku zote anachukua polisi anapokwenda kutoa fedha, sasa iweje leo (jana) aende na bodaboda kama alivyosema na eti anapofika getini akaporwa. Hayo ni maswali ya kujiuliza.

“Sasa tunachunguza hiyo ni kazi yetu. Lakini unajiuliza kila siku akienda anachukua polisi leo (jana) kaenda mwenyewe, siku zote anachukua zake leo (jana) kamchukulia na mwenzake, unampaje mtu namba yako ya siri? Kisa kina maswali, mimi ni mzoefu kwenye maswala ya uchunguzi,” alisema Kamanda Muliro.

Chanzo chetu cha habari kutoka shuleni hapo, kilidai mhasibu huyo aliyefahamika kwa jina la Bozie aliporwa jana saa 4 asubuhi wakati wa maandalizi ya sherehe za mahafali ya darasa la saba.

Mtoa habari huyo alisema pamoja na tukio hilo, eneo la shule lilikuwa shwari na mahafali yaliendelea kufanyika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles