23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Kagere aweka wazi matamanio yake

Tima Sikilo

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Meddie Kagere, amesema shauku yake ni kuhakikisha anaipigania na kuwa tishio katika Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kagere ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopia, baada ya kufunga mabao 23, leo ataiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba kuikabili UD Songo ya Msumbiji, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa utakaopigwa jijini Beira, kabla ya marudiano kuchezwa kati ya Agosti 23 na 25, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kagere alisema kama walivyokuwa na mwenendo mzuri wakati wa kipindi cha maandalizi ya msimu mpya, pia anaamini watakuwa moto kwenye Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa.

Alisema  kwa ujumla usajili wa kikosi chao ni mzuri, hivyo mashabiki wa klabu yake hiyo watarajie makubwa.

“Kwa ujumla kikosi kama ulivyokiona ni kizuri, naamini hata tutakapoingia mashindanoni Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa tutafanya vizuri.

“Binafsi nimejipanga kuipigania timu yangu ili iweze kufanya vizuri zaidi msimu ujao na mashindano ya kimataifa,”alisema Meddie Kagere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,097FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles