26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Kagera yakamilisha kuchanja dozi 45,000 za Uviko-19

Renatha Kipaka, Bukoba

Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge amesema tayari chanjo 45,000 zilizotolewa na Serikali kwa awamu ya Kwanza zimetumika na kuisha kabisa.

Meja Jen. Mbuge ametoa kauli hiyo Oktoba 13, wakati akiongea na Waandishi wa Habari mjini Bukoba.

Amesema kufanikisha shughuli hiyo ni baada ya sekta ya Afya mkoani hapo kufika kwa Wananchi na kutoa elimu shirikishi ndicho chanzo cha chanjo hizo kuisha mapema.

“Hii chanjo imekamilika kama dozi ilivyoletwa na Serikali na timu ya Afya ngazi zote zimeshirikiana na kufanikisha Michakato huo na walikuwa wakitembea nyumba kwa nyumba,” amesema Mbuge.

Amesema awali chanjo hiyo ilielekeza kutoa kipaumbele kwenye makundi maalumu ambayo ni wazee, watu wenye magonjwa sugu ambao walijitokeza kwa wingi mpaka kufikia kukamilisha zoezi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles